Jiji la Oman
Taarifa kutoka Oman zinasema kuwa watu kumi na mmoja wamehukumiwa vifungo vya miaka saba gerezani kwa kuhusika kwao na biashara ya kusafirisha watu kwa njia zisio halali.
Gazeti la Oman Observer linamnukuu afisa mkuu wa polisi wa sehemu hiyo akisema kuwa watu hao kumi na mmoja wamewaleta wanawake nchini Oman kama ni wake zao wakitumia vyeti vya ndoa bandia.
Nchi hiyo ya Oman imezindua mtandao ili kujaribu kukabiliana na kuingizwa watu nchini kwa njia za magendo na pia wameweka simu maalumu ambayo watu wanaweza kupiga ili kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji huo wa sheria. (BBCswahili.com)

1 comments:
hizi ni habari za uongo mkubwa na hata mwandishi wa habari jinsi alivyoandika kwa kiswahili naye amejihusisha na uongo wa habari hii , hakuna kitu kinaitwa kama hicho.
Post a Comment