Televisheni ya Taifa TBC 1 itaonyesha tuzo za Mamas na Zain (MTV Africa Music Awards na Zain) siku ya jumapili saa moja na nusu usiku mpaka saa tatu usiku iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa kimataifa wa Moi, kasarani jijini Nairobi nchini Kenya.Tuzo hizi zilifanyika mwishoni mwa wiki ambapo wasanii mbali mbali kutoka bara la Afrika walishindanishwa katika makundi tofauti tofauti wakiwamo wasanii kutoka Nigeria ,Kenya,congo,South Afrika,Ghana,Congo Brazaville na kwa Tanzania tuliwakilishwa na Ambwene Yesaya(AY) na Shaa.
Makundi ambayo yalishindanishwa ni pamoja na muziki wa Hip Hop, mwimbaji bora wa kike, mwimbaji bora wa kiume, mwimbaji bora wa mwaka, pamoja na video bora kwa wasanii chipukizi (My Video).
Mbali na kwamba wanamuziki kutoka Tanzania hawakuweza kupata ushindi lakini waliweza kuiwakilisha vyema Tanzania AY alipata nafasi ya kutumbuiza.Vile vile AY na Shaa walishiriki katika wimbo wa pamoja wa kumuenzi mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kimataifa Michael Jackson ambapo shoo hiyo itaonyeshwa na TBC1.
Katika kuonyesha umoja kwa wanamuzi wa Africa, MAMAS imewaunganisha na kutengeneza nyimbo mbalimbali ambapo mwanamuziki kutoka Tanzania AY ameshirikishwa na mwanamuziki kutoka Kenya Wahu na Amani na waliweza kuwateka vyema wapenzi wa muziki waliojaa katika onyesho hilo.
Wanamuziki walioimba kwenye MAMAs na Zain 2009 jukwaani siku hiyo ni pamoja na Akon, Wahu, M.I., Samini, HHP, Da L.E.S, Zebra & Giraffe, Lizha James, STL, Amani, Nameless, A.Y., Lira, 2FACE and Blu3.





0 comments:
Post a Comment