WAREMBO MISS TANZANIA WAELEZEA FAIDA ZA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII!!


Warembo wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa wamevalia kivazi kinachozungumzia kuutangaza utalii wa ndani kwanza.

Na Geofrey Tengeneza -TTB
Warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2009 wameishukuru Bodi ya Utalii Tanzania kwa kuwawezesha kutembelea baadhi ya maeneo ya vivutio vya utalii na kujionea wenyewe utajiri wa maliasili ambao Tanzania imejaliwa kuwa nao.
Wakizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa –TANAPA na Mamlaka ya hifadhi ya bonde la ngorongoro – NCAA iliyofanyika katika hoteli ya Naura Springs mjini Arusha hivi karibuni, warembo hao wamesema wamefarijika sana na kujifunza mengi yahusuyo vivutio vya utalii walivyo vitembelea na hasa ikizingatiwa wengi miongoni mwao walikuwa wakisikia tuu kuhusu vivutio hivyo na vingine na walikuwa hajapata nafasi ya kuvitembelea.
Akizungumza wakati wa chakula hicho Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bwana Geofrey Meena amsema kuwa Bodi uya Utalii Tanzania imeamua kutumia shindano hili la Miss Tanzania kuhamisiha na kukuza utalii wa ndani ambapo pamoja na kuwa mmoja wa wadhamini itatoa pia komputa laptop na fedha taslimu vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3 kwa mrembo atakaye fanikiwa kujibu uvizuri maswali yanayohusu utalii. Aidha mrembo huyoo atafanywa kuwa balozi wa Utalii wa ndani na tatatumika kikamilfu katika kampeni kamambe inayoendeshwa hivi sasa na Bodi ya Utalii ya kuhamasisha na kukuza utalii wa ndani.
Fainali za shindano hilko zinnatarajiwa kufanyika tarehe 2/10/2009 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dra es salaam na kushirikisha warembo thelethini (30) watakaopanda jukwaani na kuchuana vikali kabla ya kumpata mlimbwende wa Tanzania atakayeiwakilisha nchi kwenye shindano la dunia mwishoni mwa mwaka huu

Meneja masoko wa Bodi ya Utalii TTB Nchini Geofrey Meena akizungumza wakati wa Hafla hiyo

Mkuu wa Itifaki Miss Tanzania Albert Mqakoye na Mkurugenzi Miss Tanzania Hashim Lundenga wakicheza muziki huku warembo wakiwaangalia kwa mbali

Meneja Uhusiano wa TTB Geofrey Tengeneza kushoto akiyarudi mangoma na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment