
Basi la Singida Air Lines linalofanya safari zake kati ya Singida na Dar es Salaam likiteketea kwa moto mara baada ya kupata hitilafu ya umeme na kusababisha tairi kupasuka kitu kilichosababisha gari hilo kushika moto na kuanza kuwaka hata hivyo habari zinasema abiria walikuwa chini wakichimba dawa katika ajali hiyo watu wote salama isipokuwa dereva ambaye alijeruhiwa kutokana na tairi kupasuka wakati alipokuwa akishughulikia hitilafu hiyo ya umeme.

Polisi kutoka Singida mjini wakiwa katika eneo la tukio hata hivyo inadaiwa wamekuja katika tukio wakiwa wamechelewa kupita kiasi na walipokuja walikuwa wamesheheni silaha kuliko kifaa chochote cha kuzimia moto habari ndiyo hiyo wadau (picha kwa hisani ya Emmanuel Mgongo)
0 comments:
Post a Comment