TWANGA PEPETA KUMKUMBUKA MWALIMU J.K. NYERERE KWA KUFANYA USAFI NYUMBANI KWAKE!!

Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa Bilicanas leo kuelezea kuanza rasmi kwa maonyesho yao kwenye Klabu hiyo ya usiku ambayo yatajulikana kama Bilicanas Out of Africa Night ambayo yatafanyika siku ya jumatano kila wiki, Asha Baraka amesema bendi yake imejiandaa vyema ili kukidhi kiu ya mashabiki wake kutoka kila pembe ya jiji la Dar es salaam.
Naye Meneja matukio wa klabu hiyo Mahamed Bawazir akielezea zaidi amesema lengo la kuleta bendi tofauti katika klabu hiyo ni kuwapa wateja wake burudani tofauti kwa wakati tofauti ili kiula mmoja aweze kuridhika na kiwango cha burudani kinachotolewa na klabu hiyo ya kisasa nchini awali bendi za Akudo Impact na Fm Academia ziliwahi kutoa burudani katika vipindi tofauti kwenye klabu hiyo
Wakati huohuo katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere Mkurugenzi huyo wa ASET amesema wanamuziki wa bendi yake wamekusudia kumuenzi baba wa taifa kwa kufanya usafi maeneo yote ya nyumbani kwa Mwalimu huko Msasani, ameongeza kwamba kinachofanyika sasa ni kufuatilia taratibu zote zinazohusika ili kupata kibali cha kuwaruhusu wanamuziki hao kwa kushirikiana na baadhi ya mashabiki wenye mapenzi mema ili kumkumbuka mwalimu kwa kufanya usafi nyumbani kwake na maeneo yanayozunguka nyumbani kwa mwalimu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment