WAAMUZI WA LIGI KUU YA VODACOM WAPIGWA CHINI NA TFF!!

Fredrick Mwakalebela katibu mkuu wa Shirikisho la Soka nchini.

Shirikisho la soka nchini kupitia kamati yake ya Nidhamu limewafuta kazi waamuzi wanne waliochezesha mchezo kati ya timu ya Yanga na Majimaji mjini Songea hivi karibuni ambapo inadaiwa waamuzi wa mchezo huo walivurunda kupita kiasi.
Waamuzi waliofutwa katika ratiba ya kuchezesha michezo ya Ligi kuu ya Vodacom 2009 yote waliyokuwa wamepangiwa ni Othman Kazi mwamuzi wa kati kutoka Dar es salaam, Omary Miyaya kutoka Ruvuma, Omary Mjama kutoka Ruvuma na Kamwanga Tambwe wa Ruvuma pia, uongozi wa timu ya Yanga ya jijini ulilalamikia sana maamuzi ya marefa hao kwamba walikuwa wakiipendelea Majimaji waziwazi.
Katika kikao hicho pia kamati ya Nidhamu ya TFF imemfungia tena mchezaji Athman Idd Chuji miezi mitatu kwa utovu wa nidhamu aliouonyesha siku ya mchezo huo huko mjini Songea, Athman Idd alikuwa akitumikia adhabu nyingine ya miezi mitatu ambayo bado anaitumikia hivyo kwa kufungiwa tena na kamati hiyo miezi mingine mitatu atatakiwa kutumikia miezi sita katika adhabu yake hiyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment