Kwetu, wadau tulianza kujiuliza hii ni nini? debe ama ni kuhamasisha mashindano? Watanzania kutoka kila kona wenye haki ya kushiriki mashindano hayo wameleta wawakilishi wao, Je mameya kutoka kanda tisa nao wangetinga na vikundi vya tarumbeta hali ingekuwaje?Hii si soka, kwamba hamasa ya ushangiliaji ina nafasi yake, ndio maana kuna mechi za nyumbani na ugenini, lakini urembo tumeshuhudia Emilly Adolf mwaka 1995 akitwaa taji la Miss Tanzania akitokea Dodoma, Saida Kessy(Arusha) na Nasreem Karim anayemaliza muda wake aliyetokea Mwanza.Kwa upande wangu hii ilikuwa ni nzuri katika kuifanya kambi ya Miss Tanzania mwaka huu kuwa tofauti na miaka mingine ambapo warembo wamekuwa wakiletwa kimya kimya na kuingia kambini, lakini safari hii ilikuwa kama vile bibi harusi analetwa ukumbini ama kanisani tayari kwa kufunga ndoa si sahihi.
Hali ya jana ni kuwatia kiwewe warembo wageni Jijini Dar es Salaam kwamba wamevamia jiji la watu na wenye jiji lao wameamua kuwaleta warembo kambini ili kuwajengea mazingira ya hofu. Walichofanya waandaji wa Miss Ilala kuwapeleka warembo wao kambini si kitendo kibaya lakini kelele na mbwembwe zao, zilionekana kuwaduwaza warembo wengine waliokuwa eneo la mapokezi pamoja na wanahabari.
"Hii ni nini sasa, harusi? mshindi wa Miss Tanzania ameletwa ama niaje? ni baadhi ya maswali waliokuwa wakijiuliza watu waliokuwa eneo la mapokezi ambako mwanamama mwenye mwili mkubwa alionekana kucheza kana kwamba yupo kwenye kitchen party.
"Miss Ilala wametia fora kweli katika maandalizi yao haya na matarajio yao ni kuwa pia hata siku ya mwisho ya shindano hilo wafurahie hivyo endapo watafanikiwa kutwaa taji la Vodacom Miss Tanzania mwaka huu", mwanahabari mmoja alisikika akisifia staili hiyo ya kutinga kambini.





1 comments:
bukuku wala hakukuwa na haja ya kuponda ni aina ya shamrashara na madoido tu kunogesha shindano....kwani wagombea nafasi za uongozi kama urais,udiwani ama ubunge wanavyoendaga shamrashamra kwenye uchukuaji wa fomu huwa ni vibaya?hili ni shindano bwana kuna kushinda na kushindwa na ilala wanalitambua hilo pia,kwa upande wangu sioni cha ajabu hapo.
sijapenda ststement ya mwanamama mnene anacheza ka yuko kwenye kitchen what if yule mama angekuwa ni mama yako au dada yako hivi kweli ungeeandika hivyo....huo mchezo wakitchen party ukoje?unaendaga?
Post a Comment