UJUMBE WA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA, KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUFUTA UJINGA!!

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon.
8 Septemba 2009
Dunia yenye utajiri mkubwa, dunia ambayo elimu na weledi ni kama pasi za kumwezesha mtu kupata maisha bora, bado inakabiliwa na kiwango kikubwa na cha kutisha cha ujinga.
Takriban watu wazima 779—ambao wengi wao ni wanawake---hawana msingi unaowawezesha kusoma, kuandika au kuhesabu. Watoto milioni sabini na tano hawako shuleni. Na hata kwenye mashule, kiwango cha mdondoko wa wanafunzi ni kikubwa sana.
Lakini si kazi kubwa sana kubadili hali hiyo. Kama anavyoeleza Dk Lalage Brown, ambaye ndiye atakayetoa mada kwenye Siku ya Kimataifa ya Kufuta Ujinga ya mwaka huu: “Kujua kusoma na kuandika hata kwa kiwango cha chini kabisa kunakuwa na mchango mkubwa sana kwenye uwezeshaji wa mtu kama yeye binafsi, kijamii na kisiasa.”
Huku tukizingatia hayo, maadhimisho yanalenga zaidi kwenye kuwawezesha watu kwa kuwapa elimu. Uwezo wa kusoma na kuandika ni nyenzo zinazowezesha watu kuboresha maisha yao, kushiriki kwenye maamuzi ya kijamii, kupata taarifa juu ya afya bora, na mengine mengi. Zaidi ya hayo, kusoma na kuandika kunawawezesha watu kuelewa haki zao kama raia na binadamu.
Uwezo wa kusoma na kuandika hakuishii kwenye tendo la kusoma na kuandika tu; kunaleta heshima, fursa na maendeleo. Katika Siku hii ya Kimataifa ya Kufuta Ujinga, nawataka washirika wote kuongeza juhudi kwenye kufuta ujinga na kuchangia rasilimali zinazohitajika kupata matokeo dhahiri.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment