MSIBA UKO SINZA NYUMBANI KWAKE NA ATAZIKWA KESHO MAKABURI YA KISUTU!!

Marehemu Mohamed Mpakanjia Enzi za Uhai wake Akisali wakati wa Msiba wa Marehemu Mke wake Amina Chifupa Mpakanjia.
Mpakanja atakumbukwa sana na wadau wa muziki nchini kwani alikuwa mstari mbele sana kusaidia bendi mbalimbali ili ziweze kujikwamua kimaendeleo, na alipenda muziki na wanamuziki kitu kilichokuwa kikimfanya awe na huruma kwa wanamuziki wakati wanapokuwa na shida yoyote
FULLSHANGWE imeongea kwa simu na mmoja wa wadau wakubwa wa muziki nchini Iron Lady kama wanavyomuita huyu ni Asha Baraka Mkurugenzi wa African Stars Band ambaye ambaye yuko msibani kwa sasa maeneo ya Sinza ambako Marehemu Meddy Mpakanjia alikuwa akiishi.

Asha Baraka akizungumza kwa masikitiko amesema wamempoteza mtu muhimu katika muziki wetu hapa nyumbani kwani Mohamed Mpakanjia alikuwa msaada mkubwa sana kwa bendi zetu, kwa, wanamuziki, alitoa ushauri na pia alijitolea kwa hali na mali katika kusaidia wanamuziki na Bendi nyingi hapa nchini wakati wa uhai wake
Hivyo Umuhimu wake hautasahaulika katika mambo mengi aliyoyafanya kama mpenda maendeleo ya muziki wetu hapa nyumbani, Marehemu mpakanjia anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kisutu mishale ya saa saba mchana jijini Dar es Salaam na tutaendelea kuwaletea habari zaidi kadiri tutakavyozipata.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Dah! R. I. P my brother.

Post a Comment