MAREHEMU MOHAMED MPAKANJIA APUMZISHWA MAKABURI YA KISUTU!!

Waombolezaji mbalimbali wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Mohamed Mpakanjia kutoka nyumbani kwake Sinza Mori ili kuuweka kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda makaburi ya Kisutu kwa mazishi yaliyofanyika leo saa nane mchana huu, Marehemu Mohamed Mpakanjia alifariki jana saa 9.20 mchana katika Hospitali ya Jeshi Lugalo ambako inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu mpaka mauti yanamkuta Mungu ailaze mahari pema peponi roho ya Marehemu Amin.
Mwili wa Marehemu Mohamed Mpakanjia ukiombewa nyumabni kwake Sinza Mori.
Jeneza la Marehemu Mpakanjia likiingizwa ndani kutoka Hospitali ya Jeshi Lugalo kwa ajili ya kuuombea mwili wa marehemu tayari kuelekea makaburini kwa mazishi.
Mkwe wa Marehemu Mpakanjia Mzee Chifupa akichukua muvi wakati wa maombolezo nyumbani kwa marehemu Mpakanjia.

Kunumba Kushoto Claudi katikati na Raymond Kigosi Ray nao walikuwepo kumuaga mshikaji ambaye wamemuelezea kwamba alikuwa mtu wa watu na alikuwa mwenye kutoa msaada wa kila aina kwa wasanii na nyumba yake ilitumika mara nyingi kuigizia michezo yao hivyo marehemu Mpakanjia ameacha pengo kubwa kwa wasanii na ni kazi kubwa sana kuliziba.
Dude kushoto alikuwepo pia, laikini yeye aliendelea na mipango yake ya kuwatoka watu kama unavyomuona akiongea na simu kama vile yuko kwenye Luninga anaigiza huku wenzie wakimuangalia.
Wadau mbalimabli walikusanyika nyumbani kwame huko Sinza Mori kwa ajili ya kumuaga kwa mara ya mwisho mpendwa wao kama unavyomuona Mdau Juma Mbinzo mwenye kofia nyeupe katikati na wadau wengine.

Akina mama mbalimbali wakiwa wamekaa kwa majonzi numbani kwa marehemu Mohamed Mpakanjia.
Waombolezaji mbalimbali wakiwa nyumabni kwa Marehemu Mohamed Mpakanjia kabla ya kwenda kwenda kumhifadhi katika nyumab ya milele makaburi ya Kisutu mchana leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment