Mwimbaji Victor Aron na mtangazaji wa radio ya Praise Power anatarajiwa kuzindua Albam yake ya pili inayoenda kwa jina la Haujaanza wewe, albam hii imesheheni nyimbo zenye kuwatia watu moyo wale wenye kupitia magumu katika maisha yao laikini kutokana na kumuamini mungu wakasinda majaribu hayo.
Uzinduzi wa Albam hii ni wa poili baada ya ule wa albam ya kwanza iliyozinduliwa miaka miwili iliyopita ambayo ilikuwa ikiitwa Kurudi nyuma kwa mjinga iliyofanya vizuri sana sokoni na kumpa mafanikio makubwa katia uimbaji wake
Tamasha la uzinduzi wa albam hiyo linasimamiwa na kuandaliwa na kampuni ya Christian Directory and Consultancy Tanzania kushirikiana na yeye mwenyewe Voctor Aron kama mwimbaji ambapo uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 11/102009 kweye ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa 8.00 mchana
Victory Aron atazindua albam hiyo ikiwakatika Audio na Video sanjari na video ya kwanza ya Kurudi nyuma kwa mjinga huku akizindua pia lebo ya mavazi yake ambayo yatakuwa ni nguo za kiume kama Suti, Top za kike yaani (blauz) na fulana ambazo zitapatikana ukumbini hapo siku ya onyesho na zitauzwa kwa bei rahisi kabisa.
Waimbaji watakaomsindikiza Victir Aron siku hiyo niwaimbaji mahiri wa nyimbo za injili kama vile Christine Shusho, Bon Mwaiteje, Bahati Bukuku, Trinity Band, Jenifer Mgendi, Joseph Nyuki, Upendo na Amon Kilahiro, Ambwene Mwasongwe na Upendo Nkone na waimbaji wengine wengi ambao bado wako katika mazungumzo na Aron.
Kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa ni shilingi elfu 5.00 kwa VIP shilingi 3.000 kawaida na watoto shilingi 2.000 wapenzi wote wa muziki wa injili mnakaribishwa ili kuja kuona jinsi waimbaji wa mungu wanavyolisifu jina lake.





0 comments:
Post a Comment