Jenerali Mstaafu Robert Mboma ateuliwa tena kuwa Mweyekiti wa Bodi ya TPDC!!

Jenerali Mstaafu Robert Mboma na Mwenyekiti mpya wa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
Na Anna Nkinda – Maelezo
15/09/2009 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua tena Jenerali Mstaafu Robert Mboma kuendelea kuwa Mwenyekiti mpya wa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Julai mwaka huu hadi Juni 2012.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Alyce Tesha inasema kuwa kufuatia uteuzi huo waziri wa wizara hiyo William Ngeleja amewateua wajumbe tisa katika bodi hiyo.
Wajumbe hao ni Emanuel Ole Naiko ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha uwekezaji, Ngosha Magonya Kamishna wa fedha za nje kutoka wizara ya Fedha na Uchumi, Maduka Kessy Meneja Public Private Partnership kutoka National Development Corporation (NDC), Gosbert Blandes Mbunge wa Karagwe na Mudhihir Mudhihir Mbunge wa Mchinga,.
Wajumbe wengine ni Faida Bakari Mbunge viti maalum Pemba, Prosper Victus Kamishna Msaidizi wa Mafuta na gesi kutoka wizara ya Nishati na Madini, Mwalimu Mwalimu ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi (MUNA) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na William Haji (Mhasibu) ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Air Tanzania Corporation (ATC).

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment