MAMA SALMA KIKWETE AMKUMBUKA MWALIMU J.K. NYERERE KWA KUCHEZA BAO!!

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete leo ameshiriki kwenye uzinduzi wa mchezo wa Bao ulioandaliwa na chama cha michezo ya jadi Dar es salaam,(CHAMIJADA) Uzinduzi huo umefanya kwa kushiriki yeye kucheza Bao na Asia Ally Bushiri na hatimaye Mama Kikwete kuibuka mshindi wa mchezo huo mbele ya aliyekuwa Jaji wa mchezo Bi,Edith Dismas Lyimo (katikati) Uzinduzi huo ulifanyika kwenye viwanja vya Julius k. Nyerere Ukumbi wa Kobe Mchezo huo ni kumuenzi Baba wa Taifa Mwl, Nyerere 26.9.2009
Katika kumuenzi Baba wa Taifa Julius k Nyerere kwenye mchezo wa Bao WatotoAbdul Ally (kulia) 8yrs anayesoma darasa la pili s/msingi ugunja Zanzibar na Salim Hussein (kushoto) 9yrs anasoma darasa la tatu s/msingi majani ya chai Ilala Dar es salaam huku Man Haji akiangalia uchezaji wa Bao Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi (hayupo pichani)

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Warembo wa Miss Vodacom wakati waliposhiriki kwenye ufunguzi wa Tamasha la Chama cha Michezo ya Jadi Dar es salaam na kupiga picha ya pamoja na Warembo hao kwenye uwanja wa Maonyesho wa Julius k Nyerere PICHA NA JUMA KENGELE WA IKULU26.9.2009


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Muu wa Itifaki ya Miss Tanzania Bw. Albert Makoye kushoto pamoja na warembo wanaoshiriki katika shindano la Miss Tanzania 2009.



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment