MREMBO MISS TANZANIA AWAPAGAWISHA MAPEDESHEE, WAMMWAGIA NOTI!!

Mrembo huyu aliigiza kama mwana minenguo maarufu wa taarabu kitu kilichopelekea mashabiki na wageni waalikwa wengi waliokuwepo kupiga mayowe kwa furaha huku mapedeshee wakinyanyuka juujuu na kwenda moja kwa moja jukwaani na kuanza kumwaga manoti kama anavyoonekana Pedeshee huyu ambaye anasadikiwa kuwa ndiye aliyepagawishwa zaidi na mrebo huyo na kuanza kumwaga noti za shilingi elfu kumi kwa mfurulizo wakati mrembo huyo alipokuwa kaifanya vitu vyake jukwaani
Hili lilikuwa ni shindano la vipaji lililoshirikisha warembo mbalimbali wanaoshiriki katika shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania atakayewakilisha nchi katika shindano kubwa la Dunia hapo baadae mwaka huu, shindano la Vodacom Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika Oktoba 2 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam
Kamati ya Miss Tanznia imeeleza kuwa wanamuziki mbalimbali kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi watatoa burudani katika shindano hilo kubwa nchini, wanamuziki watakaotoa burudani katika onyesho hilo ni Koffie Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Fm Academia wa hapa nyumbani , Malow na wengine wengi.
Huyu naye siyo kwamba anacheza kungfu hapana anajaribu kuiteka hadhira iliyokuwa ikimtazama.
Siyo kwamba kachuchumaa tu hapo kiuno kinazungushwa kama pia mdau.
Huyu aliigiza kama mzazi aliyekuwa shambani akapata uchungu na kujifungua hukohuko shambani alitia fora kwa kweli.
Huyu akijinyonga vya kutosha.
Mkuu wa itifaki Miss Tanzania Albert Makoye akiwapa kipaza sauti warembo tayari kwa kuanza kujitambulisha wakati wa shindano hilo jana.

Binti Machozi Lady JayDee kushoto akiwaongoza wanamuziki Mwinyi na Joniko Mauwa wakati bendi ya Machozi ilipokuwa ikifanya vitu vyake kwenye shindano la vipaji la Vodacom Miss Tanzania ilililofanyika kweye hoteli ya Giraffe Ocean View kunduchi.

Hii ilikuwa ni Staili ya marehemu Michael Jackson iliyoporomoshwa na kundi maarufu la THT ambalo lilikonga nyoyo za mashabiki vilivyo wakati wa onyesho lao la kumuigiza Gwiji huyo wa muziki wa Pop Duniani.

Wabogojo akijipinda vilivyo yaani ilikuwa ni burudani tu.
Wadau wengine wa urembo wakiwa na nyuso za furaha katika shindano hilo haikufahamika furaha yao hasa ilikuwa ni nini, lakini yaelekea burudani ya onyesho hilo ndiyo iliyokuwa ikiwapa raha sana kama unavyoona wakiwa na nyuso za furaha kuanzia kulia ni Mkurugenzi wa magazeti ya Jambo Leo Juma Pinto, Naibu Mkurugenzi wa Jambo Leo na mwaandaaji wa Miss Temeke Benny Kisaka,Jackson Kalikumtima Mwandaaji wa Miss Ilala, Boy George Mwandaaji wa Miss Kinondoni na Afisa Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.
Wadau wa Simba Nick But kushoto na Salim Try Again walikuwepo katika onyesho hilo la vipaji ili kuona vipaji vya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania mwaka huu.
Mdau kijo wa Vodacaom na Lisa Jensen wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa onyesho hilo.


Warembo na wageni waalikwa mbalimbali wakiwa wamekaa tayari kwa onyesho la vipaji lililofanyika jana kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyoko Kunduchi jijini Dar es salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment