Mama Salma Kikwete.
27/09/2009
Mke wa Rais, SALMA KIKWETE atafungua rasmi mashindano ya mpira wa Netiboli yanayozishirikisha nchi 10 za Afrika Jumatatu ijayo tarehe 28 Septemba katika uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi amezitaja nchi zitakazoshiriki kuwa ni Afrika Kusini, Kenya, Uganda, Malawi,Zambia,Lesotho, Namibia, Zimbabwe, Swaziland na wenyeji Tanzania.
Anna Bayi amesema katika siku ya ufunguzi kutakuwa na mechi mbili ambapo mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Tanzania na Lesotho na wa pili kati ya Malawi na Kenya. Mechi hizo zitaanza mara baada ya ufunguzi wa michuano hiyo majira ya saa sita mchana.
Kwa mujibu wa Anna Bayi kesho wachezaji wa timu zitakazokuwa zimewasili watatembelea vituo vya watoto yatima vya Msimbazi na Kurasini, saa nane mchana.
Miongoni mwa viongozi watakahudhuria ufunguzi huo ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, mabalozi kutoka nchi za Afrika Kusini, Malawi, Kenya, Uganda, Zambia na Zimbabwe.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam John Lukuvi wakurugenzi wa mashirika yanayodhamini michuano hiyo pamoja na wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.

0 comments:
Post a Comment