HEKO SERENGETI BOYS, YAWASILI NA MEDALI YA SHABA.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo asubuhi majira ya saa 3 kwa shirika la Ndege la Kenya, baada yakuifunga wenyeji Sudan 2-0 na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu huku wakitwaa medali ya shaba na Dola za Kimarekani 5000 FULLSHANGWE tunaipongeza timu hiyo kwa kufikia nafasi hiyo kwani kila kitu huwa kinakwenda kwa hatua hivyo sisi tunaona hii ni hatua nzuri lakini pia tunawataka wachezaji wote kuzingatia mazoezi, nidhamu na kujituma kwani ndiyo njia pekee inayoweza kuwapeleka kwenye mafanikio kama vile kaka zao akina Henry Joseph, Nizar Khalfan na Nadir Haroub Canavaro ambao angalau wanaanza kuonyesha njia ya mafanikio kwa soka la kulipwa kwa wachezaji wa bongo.
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuwapokea wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana Serengeti Boys leo asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa timu ya Vijana ya Serengeti Boys wakipiga picha ya pamoja na meneja uhusiano wa Serengeti Breweries Teddy Mapunda wa tatu kutoka kushoto mara baada ya timu hiyo kuwasili ikitokaea Sudan ilikoshiriki kombe la Chalenji kwa vijana na kushika nafasi ya tatu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment