WAWAKILISHI WA ERITREA MISS EAST AFRICA 2009 HAWA HAPA!!

cefora
selemawit

02nd September, 2009
Mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa mwaka huu, yameingia katika sura mpya baada ya Nchi washiriki kuanza kupata wawakilishi wake katika mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 18 December, 2009 jijini Dar es salaam, Tanzania.
Nchi ya kwanza kutangaza warembo wake ni Eritrea ambayo tayari imepata wawakilishi wake watakao iwakilisha Nchi hiyo katika mashindano hayo mwaka huu.
Warembo hao walipatikana katika mashindano ya kuvutia ya urembo yaliyofanyika jijini Asmara Nchini humo hivi karibuni.
Warembo watakaoiwakilisha Eritrea katika mashindano ya mwaka huu ni
1. Selamawit Zerabruck Ghebreslassie
Date of Birth 19-08-1991
Height 172
Hobbes reading, Traveling, movies
2. Sefora Messele Ghebreezgabiheir
Date of Birth 19-09-1991
Height 180
Hobbes swimming, reading
Mwaka jana Nchi ya Eritrea pia ilikuwa ya kwanza kutangaza wawakilishi wake katika mashindano ya Miss East Africa 2008 yaliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ambapo iliwakilishwa na warembo Rahwa Ghebrehiwet pamoja ya Menal Hussien ambapo Rahwa Ghebrehiwet alifanikiwa kuibuka mshindi wa tatu.
Mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa huandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.
Nchi 14 za ukanda wa Afrika mashariki tayari zimeshathibitisha kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ambazo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, zingine ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, visiwa vya Seychelles, Re union, Madagascar, Comoros na Mauritius.
Wakati huohuo ile bahati nasibu ya Miss East Africa ya kuchangia yatima ambapo mshindi wa kwanza atajishindia gari jipya aina ya Range Rover sport inaendelea
na watu wote wameombwa kushiriki bahati nasibu hiyo.
“Tunawaomba watu wote washiriki kwa kuandika neno SHINDA kwa kutumia simu zao za mkononi na kutuma kwa sms kwenda namba 15567 ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali na wakati huohuo wakichangia yatima wa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla”

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment