Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje Ulinzi na Usalama Wilison Masilingi katika ufunguzi wa maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45 hivi karibuni. Mh. Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yaliyofungwa rasmi leo na waziri wa ulinzi Dr. Hussein Mwinyi wa kwanza kulia, katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing ,Ukonga jijini Dar es salaam, na kushoto ni Naibu wake Dkt. Emannuel Nchimbi
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam.
Serikali imelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa hatua liliyochukua ya kuwakaribisha wananchi ili kuona kazi na shughuli mbalimbali zinazofanywa na jeshi hilo hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa kufunga wiki ya maonyesho ya miaka 45 ya JWTZ yaliyofanyika katika viwanja vya kikosi cha 603, Air wing jijini Dar es salaam.
Amesema hatua hiyo imewapa fursa wananchi kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na vikosi mbalimbali vya jeshi la Wananchi vikiwemo vikosi vya anga,ardhini na majini.
“Maonyesho mliyoandaa yanatoa fursa ya wananchi kuja huduma zinazotolewa na jeshi letu nah ii ni nafasi pekee kwa wananchi kuwa karibu na Jeshi lao na kupata nafasi ya kujifunza umoja na utendaji wa kazi na kwa mwaka huu hii ni hatua nzuri kwa viongozi wa jeshi letu kuanzisha mfumo huu” amesema.
Amefafanua kuwa wananchi wengi wamejifunza na kupata huduma mbalimbali za afya,huduma na ufafanuzi katika masuala ya ujenzi,kilimo, elimu, ulinzi na huduma za uokoaji na utoaji wa misaada wakati wa majanga mbalimbali yanayotikea nchini.
Kuhusu historia ya JWTZ katika Bara la Afrika Dkt. Mwinyi amesema jeshi hilo lina historia ndefu ndani na nje ya nchi ikiwemo historia ya ukombozi wan chi za kusini mwa Afrika,harakati mbalimbali za kusaidia kupigania uhuru kwa nchi za Afrika zikiwemo Afrika kusini, Msumbiji, Zimbabwe na pia Jeshi la wananchi kupata ushindi katika vita dhidi ya nduli Iddi Amini wa Uganda.
Pia amesema JWTZ imelijengea heshima taifa letu kutokana na mchango mkubwa linaloutoa katika kushiriki katika kuleta amani katika mataifa mbalimbali barani Afrika na pia mchango wake katika majeshi ya Umoja wa matifa ya kulinda amani nchini Sudan.
Kwa upande wake mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange amesema Jeshi lina mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa linajenga mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa askari wake na pia kuwajengea uwezo zaidi kielimu katika ngazi mbalimbali zikiwemo shahada,stashahada, shahada za uzamili na uzamivu ili kuboresha utendaji kazi na nidhamu na pia uaminifu wa hali ya juu miongoni mwa askari.
Kuhusu tatizo la baadhi ya wanajeshi wanaokiuka taratibu na sheria za jeshi Generali Mwamunyange amesema wapo baadhi ya wanajeshi wachache sana ambao wanakosa uadilifu na kujikuta wakitenda na kushiriki vitendo vya kihalifu na kukiuka maelekezo mbalimbali yanayotolewa.
Naye Mkuu wa Jeshi la Anga la Afrika ya kusini Luteni Generali Carlo Gagiano ameisifu Tanzania kwa juhudi inazochukua na mchango wake katika kulinda na kudumisha amani katika nchi mbalimbali za Afrika.
Katika wiki ya maonyesho ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania shughuli mbalimbali zimefanyika na watu mbalimbali wamejitokeza kupima afya zao na kupata matibabu ya macho, kupatiwa miwani, tiba ya meno ,kupata dawa za magonjwa mbalimbali na pia utoaji wa hiari wa damu na kupima VVU.

0 comments:
Post a Comment