ALBERT MNALI KUMVAA WAZIRI MATHIAS CHIKAWE NACHINGWEA!!

Albert Mnali akikabidhi baiskeli kwa wakazi wa Bukoba alipokuwa mkuu wa Wilaya hiyo.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh Albert Mnali ametangaza nia yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Nachingwea kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akimvaa Mbunge wa sasa wa jimbo hilo Mathias Chikawe ambaye ni Waziri wa Sheria na Katiba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Albert Mnali ambaye Rais Jakaya Kikwete alimvua madaraka na kumtimua kazi mwanzoni mwa mwaka huu akiwa mkuu wa Wilaya ya Bukoba, kutokana na kitendo chake cha kuamrisha kuchapwa bakora hadharani waalimu wa shule za msingi za Katerero, Kanazi na Kasenene kwa sababu zilizoelezwa kushindwa kuwajibika na kufanya shule hizo zidorore katika masomo.
Akizungumza kwa njia ya simu asubuhi ya leo jijini Dar es salaam, Mh.Albert Mnali amesema sasa ameamua kugeukia katika upande mwingine wa siasa akiamini kuwa ataweza kuchangia vyema mawazo yake akiwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha watanzania wa Jimbo la Nachingwea.
Mwaka 2005 Albert Mnali aligombea katika jimbo hilo na kushika nafasi ya pili katika kura za maoni za chama hicho na kuzidiwa na mbunge wa sasa Mh. Mathias Chikawe

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment