Elimu ya dini na elimu ya mazingira vikichanganywa kwa pamoja nchi itapata maendeleo!

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia) akipokea zawadi ya nakala za misahafu kutoka kwa Dr. Abdel – Baqi (kushoto) wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an tukufu yaliyofanyika katika Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam . Mashindano hayo yaliandaliwa na ubalozi wa Misri kupitia kituo chake cha utamaduni kiitwacho Egyption Islamic Center na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Dar es Salaam.

Na Anna Nkinda – Maelezo

Elimu ya dini na elimu ya mazingira vikichanganywa kwa pamoja nchi itapata wataalamu wa hali ya juu ambao watasaidia kuleta maendeleo ya nchi..


Hayo yamesemwa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na washiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an tukufu yaliyofanyika katika Hoteli ya Movenpick iliyopo jijini Dar es Salaam.


Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka waandaaji wa mashindano hayo ambao ni ubalozi wa Misri kupitia kituo chake cha utamaduni kiitwacho Egyption Islamic Center kilichopo Chang’ombe na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Dar es Salaam kuona umuhimu wa kujenga kituo kama hicho katika mikoa mingine.


“Kituo hiki kipo hapa Dar es Salaam tu na Tanzania ni kubwa nawaomba hapa pawe makao makuu na katika maeneo mengine hapa nchini mjenge vyuo vingine ili huko nako vijana wapate elimu ya dini ambayo itawasaidia katika maisha yao”, alisema Mama Kikwete.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment