MISS UTALII TANZANIA WAULA MISS UNITED NATIONS!!

Bw. Gideon Chipungahelo akiongea na warembo walioshiriki Miss Utalii Tanzania mwaka jana.

Kwa mara nyingine tena,katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni kukubalika zaidi kimataifa kwa waandaaji na mashindano ya Miss Utalii Tanzania,
Rais wa Miss Utalii Tanzania Gideon Erasto Chipungahelo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Taifa na mwakililishi pekee hapa Tanzania wa mashindano ya Dunia ya Miss Umoja wa Mataifa.
Uteuzi huo umefanywa na Rais wa Dunia wa Mashindano hayo Kathryn Pettit,kupitia kwa mkurugenzi wa Dunia wa mashindanio hayo Leon Williams.Kwa uteuzi huo washindi wa Taifa wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania watawakilisha Tanzania katika fainali za dunia za mashindano hayo kuanzia mwaka huu.
Huu ni uteuzi wa Tatu wa kimataifa kwa Ndugu Chipungahelo kushika nyadhifa za kimataifa za mashindano ya urembo. Nyadhifa nyingine alizo nazo ni pamoja na Rais wa Dunia wa Mashindano ya Miss Heritage World,Mkurugenzi wa bara la Afrika wa Miss Tourism World organization na mkurugenzi wa taifa wa International Miss Tourism world Pageants.
Hii inamanisha kuwa sasa washindi wa Taifa wa Miss Utalii Tanzania ,watakuwa wanawakilisha Tanzania katika mashindano matatu tofauti ya Dunia ambayo yanalenga katika kutangaza utalii,pia itakuwa ni fulsa ya pekee kwa warembo wa Miss Utalii Tanzania kupeperusha bendera ya Tanzania na kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kimataifa.
Bodi ya wakurugenzi inajivunia kupata fulsa hizi za kujivunia na za pekee ambazo zitatoa mchango mkubwa kwa miss utalii Tanzania kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali ya awamu ya nne ,Mamlaka ya Hifadhi za taifa na nchi kwa ujumla ya kuinua pato la taifa litokanalo na utalii kwa kutangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii hususani Hifadhi za taifa hasa katika kipindi hiki cha mtikisiko wa uchumi wa Dunia.
Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia ya Miss Umoja wa Mataifa(Miss United Nations)yenye makao yake makuu nchini marekani,Miss utalii dunia (Miss Tourism world) yenye makaoyake makuu nchini Uingereza,Miss International Tourism Pageant yenyemakao yake makuu marekani na Miss urithi wa Dunia (Miss heritage world) yenye makao yake nchini Uturuki na Tanzania,watapatikana katika fainali za Taifa za Miss utalii Tanzania ,ambazo waandaaji wake pekee ni Miss Tourism Tanzania Beauty Pageant Limited chini ya bwana Gideon Chipungahelo,ambazo zitafanyika mwezi Novemba baada ya kukamilika fainali za mikoa na kanda zinazoendelea hivi sasa chini ya mawakala wetu nchi nzima.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment