VITUO VYA MISAADA YA KISHERIA NCHINI VYATAKIWA KUTOA HUDUMA MAENEO YA VIJIJINI.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora George Mlawa akiongea na washiriki wa kongamano la Kitaifa la siku mbili la wasaidizi wa Kisheria linaloendelea jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa- MAELEZO.
Dar es salaam.
Changamoto imetolewa kwa vituo vya misaada ya kisheria nchini kuhakikisha kuwa vinawafikia na kuwasaidia wananchi wengi wanaoishi maeneo ya vijijini ili wajue haki zao.
Wito huo umetolewa leo na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora George Mlawa wakati wa kongamano la Kitaifa la wasaidizi wa Kisheria linaloendelea jijini Dar es salaam.

Amesema vituo vingi vya misaada ya kisheria viko maaeneo ya mijini jambo linalosababisha wananchi wengi wanaoishi katika maeneo ya mijini kupata msaada wa kisheria kwa haraka zaidi tofauti na wale wanaoishi maeneo ya vijijini.
“Vituo vingi vya misaada ya kisheria kwa sasa viko mijini wakati katika maeneo ya vijinini ambako msaada wa kisheria na uelewa wa wananchi ni kuhusu sheria ni mdogo na wakati mwingine vituo vya sheria viko mbali sana” amesema.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment