Muimbaji wa nyimbo za injili wa jijini Mwanza,Esther Tindosi Kusekwa anatarajia kuzindua albamu yake mpya itakayoitwa Faraja kwa yatima na wajane, mnamo Agosti 29 katika uwanja wa Kambarage,mjini Shinyanga naAgosti 30 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwaza.
Uzinduzi huo ambao unaratibiwa na kampuni ya Flora TalentPromotions,chini ya Mkurugenzi wake Bi.Flora Lauwo ,utakuwa ni wapekee na wenye kuwasisimua wapenzi wa muziki huo wa kiroho ambao kwasasa umekuwa ukikubalika na kupendwa kwa kiasi kikubwa.Bi.
Flora amesema kuwa albamu itakayoziduliwa itakuwa na jummla yanyimbo nane, ambazo kwa kuzitaja chache ni Faraja kwa yatima na wajaneuliobeba albamu nzima,nagalolela ambao umeimbwa kwa lugha yakisukuma,Kemea,Ole wao,Akina mama,Dhambi,Nimechoka na nyinginezo."Watakaousindikiza uzinduzi huo atakuwepo muimbaji mahiri wa muziki wakiroho kama vile Joseph Nyuki,Mchungaji Baru,Jerusalem Band,MathaRamadhani,Kwaya ya Vijana wa Bwiru, Kwaya ya AIC Makongoro bilakumsahau Bi Josephin anayetamba na wimbo wake wa mateso ya mwenyehaki, na band nzima ya Tabata ambao wanatamba na wimbo wao wa natembeakidogo kidogo, nikinyatanyata,Na wengine weeeeengi."amesema Flora.Flora amesema kuwa katika suala la maandalizi kila kitu kinakwendasawa mpaka sasa,na kwamba kiingilio kimepangwa kuwa shilingi 1000/= kwa watoto na watu wazima kuwa ni shilingi 2000/=.
0 comments:
Post a Comment