Maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45 yafana!!.

Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje Ulinzi na Usalama Wilison Masilingi mara baada ya ufunguzi wa maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh. Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yanayoendelea katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing ,Ukonga jijini Dar es salaam.Wa kwanza Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein mwinyi ambaye aliambatana na Naibu wake Dkt. Emannuel Nchimbi (wa kwanza kushoto).
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje, Ulinzi na Usalama Mh. Wilson Masilingi akipata ufafanuzi kutoka kwa Luten Kanali Anselum Bahati kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na JWTZ kikosi cha Nyumbu wakati wa maonyesho ya miaka 45 ya JWTZ.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye maonyesho ya JWTZ kutimiza miaka 45 wakipata huduma za tiba na ushauri leo katika mabanda ya Maonyesho katika viwanja vya kikosi cha 603 cha Jeshi la wananchi Air wing,Ukonga jijini Dar es salaam.


Matukio mbalimbali katika picha kuhusu wiki ya maadhimisho ya miaka 45 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yanayoendelea katika viwanja vya jeshi kikosi cha 603, Airwing,Ukonga jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.









You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment