Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo PPF Tower kuhusu mashindano ya kuendesha Baiskeli yatakayofanyika Oktoba 25 mkoani Mwanza na kushirikisha makundi matatu ya waendesha Baiskeli, kundi la kwanza wanaume watakaokimbia km 150, kundi la pili wanawake watakaokimbia km80 na kundi la mwisho la walemavu litakalokimbia na baiskeli km10
Rukia amesema washiriki wote watajigharimia usafiri kutoka maeneo mbalimbali wanayotoka na kufika katika eneo la kituo cha mashindano jijini Mwanza pia watajigharimia chakula na malazi wakati wote watakapokuwa mkoani mwanza kwa mashindano.
Fomu za kushiriki katika mashindano hayo zinapatikana katika maduka yote ya Vodashop yaliyopo Nyamagana, Nyerere Road, PPF Tower Mwanza, Shinyanga, Tabora, Dodoma na Zanzibar fomu pia zinapatikana katika ofisi za CHABADA na vituo vingine vitakavyotangazwa hapo baadae katika picha kulia ni Nizar Manji wa CHABADA na kushoto ni Arnold Kileo Meneja Bidhaa na Utafiti Vodacom Tanzania.
0 comments:
Post a Comment