AURORA KUSAIDIA MISS UTALII TANZANIA 2009-TEMEKE

Erica Allan(23)
Happy Felix(22)

Kampuni ya Ulinzi ya Aurora ya jijini Dar es Salaam, imejitokeza kusaidia shindano la miss Utalii Tanzania 2009-Temeke litakalofanyika tarehe 25 Sep katika Ukumbi wa City Garden (Zamani Gerezani) ,Kariakoo Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Aurora Ally Aurora alisema jana kuwa wanatazamia kukutana na kamati ya miss Utalii Tanzania 2009-Temeke, siku ya jumatatu ambapo watakubaliana Sehemu Muhimu za Kusaidia ikiwemo suala zima la Usafiri wa kuwawezesha washiriki kwenda katika Vivutio vya Utalii vya Taifa kwa lengo la kujifunza Zaidi."nitawapa usafiri kwani nafikiri hilo ndilo litakuwa suala la kwanza kwao ili waweze kutembelea Hifadhi za Utalii za Taifa ambako watajifunza masuala mengi yanayoihusu nchi yetu,pengine kama kutakuwa na jambo limgine la muhimu pia tutazungumza nao lakini kikubwa nahaidi kuwasaidia ili kufanikisha shindano hili"alisema auroraMashindano ya Miss Utalii Temeke 2009, ni mashindano yanayolenga kumtafuta Balozi wa kutangaza, kuibua na kuhamasisha vivutio vya Utalii,Utalii, Utamaduni, Utalii wa Ndani, na Mianya ya Uwekezaji katika Wilaya ya Temeke 2009.Shindano hili pia linalenga kuwapata washindi watakaowakilisha wilaya ya Temeke katika fainal za Miss Utalii Tanzania 2009-Kanda ya Mashariki ambayo yatajumuisha washindi kutoka wilaya za Kinondoni,Temeke, Ilala, Mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Lindi, na Mtwara..
Shindano la Miss Utalii Tanzania 2009-Temeke , Limeandaliwa na Linda Masanche (Miss Utalii Tanzania 2005-Vipaji, ambalolimepangwa kufanyika siku ya ijumaa Sept 25-2009 katika Ukumbi wa City Garden Club Gerezani Kariakoo(zamani Gerazani Clabu). jumla ya Warembo 15 wanatarajia kupanda jukwaani katika Ukumbi huo unaomilikiwa na Paradise Group of Company ya jijini ambao ni wamiliki pia wa Paradise Hotel Bagamoyo, Tansoma Hotel ya Dar es Salaam, City Garden, Dar es Salaam Conference Centre na East Afrika Hote y Arusha.shindano hilo linalotajwa kuwa la pekee na historia katika Wilaya ya Temeke 2009 wakiwemo Klabu ya kisasa ya Kitalii ya City Garden Club Gerazan, Aucland Tours &Travel Kampuni inayomilikiwa na mfanya biashara maarufu nchini Malijani Msofe(Papaa Msofe), Monalisa Feneture & Tiles wauzaji wa samani vya kisasa, Hatman Production,Varry Spring, Mbuge wa Wilaya ya Temeke Abbas Mtenvu,na Mbunge wa Wilaya ya Kinondoni Idd Azan

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment