Kesi ya suruali ndefu yaanza Sudan !!

Lubna atacharazwa viboko 40 endapo atakapatikana na hatia.

Kesi hiyo iliahirishwa wiki iliyopita baada ya Lubna kuomba ajiuzulu kwanza wadhifa wake kama mfanyikazi wa Umoja wa Mataifa.
Wadhifa huo ulimpa kinga ya kutoshitakiwa lakini mwandishi huyo wa habari alitaka kukabiliana na sheria vilivyo na hata kuibadilisha.
Kwa mujibu wa sheria za Sudan, Lubna atacharazwa viboko 40 endapo atakapatikana na hatia.
Mwandishi huyo wa habari aliwaalika watu 500 kuhudhuria kesi yake alipofikishwa mbele ya mahakama tarehe 29 July.
Hapo ndipo aliambia mahakama, "ningependa kujiuzulu kutoka UN kwa sababu ningependa kesi hii iendelee."
Lubna alikamatwa pamoja na wanawake wengine kwa kukosa adabu kutokana na mavazi yao.
Baadhi ya wanawake hao walitandikwa viboko 10 kila mmoja na kutozwa faini. Miongoni mwao walikuwa wanawake ambao sio waumini wa dini ya Kiislamu.
Lakini Lubna na wanawake wengine wawili washtakiwa waliomba kuwakilishwa na wakili, hatua ambayo ilikawisha kesi yao.
Lubna anadai kwamba hajatenda kosa lolote chini ya sheria za Kiislamu ingawa kuna kipenge katika sheria za nchi hiyo ambacho kinapinga mavazi yasiyostahiki habari na www.bbcswahili.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment