Maandalizi ya Tamasha la Timu ya Simba Sports Club linalotarajiwa kufanyika tarehe 8 Agosti yanaendelea vyema, akizungumza na waandushi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye Mgahawa wa Hadees Mwenyekiti wa Klabu hiyo Mzee Hassan Dalali katikati, amesema tamasha litaanza saa 12 asubuhi ambapo milango itakuwa wazi na kutakuwa nashughuli mbalimbali za Burudani.
Mgeni wa heshima anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samweli Sitta huku waalikwa mbalimbali wakiwemo wabunge na mawaziri na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu wakihudhuria katika, ambapo kutakuwa na mechi ya utangulizi kati ya timu ya simba U20 na Africa Lyon U20 na baadae itafuatia mechi katika ya Simba na Sports Club Villa ya Uganda ambayo inatarajiwa kuwasili nchini tarehe 6 Agosti
Katika Tamasha hilo kutakuwa na ugeni kutoka Norwey wanaotoka katika Timu anayochezea mchezaji Henry Joseph aliyekuwa akiichezea timu ya Simba kabla ya kununuliwa na timu hiyo wageni watakaokuja kutoka Norwey ni Rais wa timu hiyo Henrik Mohn, wkala wa fifa Glenn Shiller na Azzedin Soud wa Grand Canaria Football Centre ya Norwey ambao nao pia watawasili tarehe 6 agosti, Tiketi zitauzwa kati ya shilingi 50.000 VIP , 20.000 Main Stand,8.000 Green Stand na 3.000 mzunguko. walioko katika picha ni Mwina Kaduguda katibu mkuu Simba Kushoto na Mratibu wa Tamasha Mulamu Ghambi aliyeko kushoto
0 comments:
Post a Comment