ABDALLAH ZOMBE NA WENZAKE WAKO HURU, PATA MATUKIO KATIKA PICHA!!

Abdalla Zombe akiingia kwenye Gari tayari kurudi nyumbani mara baada ya kuachiwa huru yeye pamoja na wenzake 9 ambao walikuwa waktuhumiwa kwa kesi ya kuwauwa wafanyabiashara watatu kutoka mkoani morogoro, Jaji Salum Masati aliyekuwa akisoma hukumu hiyo iliyochukua takriban masaa saba na zaidi katika kuhitimisha hukumu hiyo, amesema watuhumiwa hawana hatia kwakuwa serikali imeshindwa kuthibitishia mahakama juu ya tuhuma zilizokuwa zikiwakabili washitakiwa hivyo mahakama inawaachia huru watuhumiwa wote wako huru kuanzia sasa
Aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar es salaam Abdallah Zombe akisindikizwa na makachero mara baada ya kuachiwa huru na mahakama kuu ya Tanzania baada ya kutopatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili pamoja na wenzake 9.

Magari ya Polisi yakiwa tatayri kabisa ili kuwatoa Zombe na Wenzake mahakamani hapo ilibidi watolewe na magari ya polisi kwa usalama zaidi kutokana naumati uliokuwa umefurika mahakamani hapo ili kusikiliza hukumu hiyo.

Wakili wa Upande wa Serikali Jasson Kashozi akihojiwa na wanahabari mwara baada ya hukumu ya Zombe na waenzake 9 ambao wameachiwa huru na mahakama kuu baada ya kutopatikana na hatia jioni hii kutokana na mashitaka ya mauaji ya wafanyabiashara watatu iliyokuwa ikiwakabili.

Ndugu jamaa na marafiki wa waliokuwa watuhumiwa wa mauaji ya wafanyabiashara watatu kutoka mkoani Morogoro wakishangilia mara baada ya ndugu zao kuachiwa huru katika mahakama kuum ya Tanzania leo jijini Dar.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment