Rais Jakaya Kikwete akimuaga Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Margaret Chan mara baada ya kuzungumza naye Ikulu ndogo, Chamwino Dodoma. Dkt Chan alirejea jijini Dar es salaam kuendelea na ziara yake.
Mganga mkuu wa Manispaa ya Ilala Dafroza Lymo akitoa maelezo kwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Margaret Chan kuhusu huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo wakati alipoitembelea hospitali hiyo jana jijini Dar es salaam.Mstari wa nyuma (katikati) ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Margaret Chan akipokea maelezo kutoka kwa madaktari kuhusu huduma zinazotolewa kwa akina mama na watoto katika moja ya wodi alizotembelea katika hospitali ya Amana jana jijini Dar es salaam.Dkt Chan alitembelea hospitali hiyo kujionea juhudi mbalimbali zinazofanya katika kupambana na Malaria,utoaji wa huduma ya mama na mtoto,utunzaji na utoaji wa madawa kwa wagonjwa.
0 comments:
Post a Comment