Dr. Sayoki G Mfinanga, MD,PhD mkurugenzi wa Muhimbili Medical Research Centre, National Institute for Medical Research (NIMR) akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo juu ya kuimarisha watafiti na tafiti mbalimbali zinazofanyia katika ukanda huu wa Afrika
Taasisi kumi na nane za Kiafrika zitashiriki katika Mpango wa Wellcome Trust utakaohusisha Mashirika saba ya Kimataifa utakaogharimu paundi milioni 30 kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa kitafiti barani Afrika. Ushirika wetu, “Ushirika wa Afrika wa Utafiti wa Mfumo wa Ekolojia na Afya ya Binadamu na Wanyama” utapata jumla ya pauni milioni nne na laki saba (4,700,000) kwa kipindi cha miaka mitano. Tanzania itapata kiasi kikubwa zaidi kwa sababu taasisi kuu 5 (kati ya 11 zilizounda ushirka huu) ni za hapa nchini.
Wellcome Trust ni Taasisi inayojitegemea ambayo hufadhili tafiti zinazolenga kuboresha afya ya binadamu na wanyama. Nchini Uingereza, Wellcome Trust ni chanzo kikubwa kuliko vyote visivyokuwa vya kiserikali vinavyofadhili tafiti za kitiba. Shughuli yake kuu ni kukuza na kuendeleza tafiti kwa lengo la kuboresha afya ya binadamu na wanyama. Ushirika huu wa (Utafiti wa Mfumo wa Ki-ekolojia) unahusisha njia nyingi na za aina tofauti katika kupanua wigo wa fasiri za afya zilizozoeleka, ukizingatia umuhimu wa mahusiano kati ya shughuli za kibinadamu, mabadiliko ya ki-ekolojia na afya, na kushirikisha mitazamo muhimu ya kijamii na kiuchumi. Ushirika utashughulikia masuala mapana ya Mfumo wa Ekolojia-Afya, hasa ukilenga epidemiolojia na udhibiti wa magonjwa ya wananyama yanayoweza kuwapata binadamu, na kubuni mikakati thabiti ya kudhibiti magonjwa haya.
Taratibu za Kitaasisi: Ushirika huu unashirikisha Vyuo Vikuu 7 na Taasisi 4 za Utafiti kutoka nchi 6 za Afrika Magharibi na Mashariki (Côte d’Ivoire, Senegali, Chadi, Ghana, Tanzania na Uganda) na wabia 3 wa nchi za Ulaya (Taasisi ya Kitropiki ya Uswisi na Vyuo Vikuu vya Glasgow UK na Bergen, Norway). Ushirika unajumuisha taasisi za taaluma za tiba ya binadamu na wanyama na pia uwakilishi wa nchi zinazoongea Kifaransa na Kiingereza.
Taasisi kuu tano za Tanzania ambazo ni wanachama wa Ushirika huu ni Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (yaani National Institute for Medical Research, NIMR) (Kituo cha Muhimbili), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shiriki-Muhimbili, na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani) na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (yaani Tanzania Wildlife Research Institute, TAWIRI). Taasisi zingine shiriki ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hebert Kairuki na Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin (SAUT) iliyoko Bugando-Mwanza.
Muundo wa Utawala: Ushirika unajumuisha watalaamu wa afya ya wanyama na binadamu kutoka Vyuo Vikuu na Taasisi za Utafiti mbali mbali za Afrika, kutoka mataifa yanayozungumza Kiingereza na Kifaransa. Mkurugenzi wa Ushirika atakuwa Dkt. Bassirou Bonfoh (Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya Sahel, Cote d’Ivoire). Atasaidiwa na wakurugenzi wasaidizi wawili (kutoka vyuo vikuu au taasisi za utafiti) kutoka Afrika Mashariki na Magharibi: 1) Dkt. Sayoki Mfinanga kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, Tanzania, na 2) Prof. Fantondji Agathe Togbé, kutoka Chuo Kikuu cha Abobo-Adjame, Cote d’Ivoire. Wakurugenzi hawa pamoja na mwakilishi mmoja mmoja kutoka kila chuo/taasisi nyingine mwanachama wa Ushirika watakuwa ndiyo timu ya menejementi itakayoratibu shughuli za pamoja kwa Afrika Mashariki na Magharibi.
Upeo wa Ushirika: Kwa kifupi, Ushirika huu unalenga kujenga uwezo wa kitafiti (katika Afrika) na kukuza kundi la watafiti mahiri wenyekumudu ushindani wa kimataifa katika nyanja za mfumo wa ekolojia-afya katika Afrika. Ushirika utafanikisha hayo kwa kuwajengea uwezo kikazi wanasayansi vijana wa Kiafrika. Katika Afrika, changamoto kubwa kuliko zote kwa mwanasayansi (au mtafiti yeyote) katika kufikia kiwango cha juu kabisa na kujiita (au kuitwa) mtafiti mahiri wa kimataifa, huwa ni kutambuka kutoka kuwa mhitimu wa shahada ya udaktari ya falsafa na kujijenga kitaaluma ili atambulika kimataifa.
Kwa kupata ufadhili huu wa Welcome Trust, lengo kuu la Ushirika huu ni kuanzisha programu 11 za utafiti zenye lengo la kutoa nafasi za kushiriki ama kuongoza tafiti hizo kwa walihitimu wapya wa shahada ya udaktari wa falsafa wenye kuonyesha kipaji cha juu kabisa. Wale watakaofuzu kupata nafasi hizo watawezeshwa kuendesha tafiti hizo ili kukuza zaidi vipaji vyao na kujisimika kwenye ulimwengu wa kitafiti kimataifa. Katika kukuza ujuzi wa kitaaluma, utaziwezesha taasisi shiriki kubadilishana wanasayansi (yaani mwanansayansi mmoja mmoja kutoka taasisi moja kwenda taasisi nyingine) kwa mafunzo ya muda mfupi, kufanya utafiti au kufundisha. Ushirika pia utatoa nafasi chache kwa ajili ya wanafunzi wa udaktari wa falsafa. Malengo mengine ni pamoja na kujenga uwezo wa menejimenti za utafiti; kutumia matokea ya tafiti ili kuboresha sera za kudhibiti magonjwa husika; kufanya mikutano na makongamano ya pamoja na kuboresha miundo-mbinu ya utafiti ikiwa ni pamoja na kupata vifaa vya kisasa.
Masuala muhimu yanayojumuishwa katika mfumo wa ekolojia-afya ni pamoja na:
Magonjwa mapya yanayoibuka na magojwa ya wanyama yanayoweza kuwaathiri binadamu,
Mwenendo wa maambukizi wa magonjwa katika mazingira ya mfumo wa ekolojia unaobadilika kwa kasi (mijini na vijijini),
Madhara ya mfumo wa mawasiliano ambao umepelekea dunia kuwa kama kijiji na kuongezeka kwa kasi ya usafirishaji wa binadamu na wanyama. Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya masuala yaliyotajwa hapo juu na ueneaji wa kasi wa maradhi yanayoibuka (au hata ya mlipuko) zama hizi (k.m. homa ya bonde la ufa, homa ya mafua makali au ya ndege, mafua ya nguruwe na hata malaria). Mambo haya yanafanya swala la kuwa na ufahamu wa hali ya juu kuhusu mfumo wa ekolojia na mahusiano ya viumbe, hasa kati ya wanyama na binadamu, kuwa muhimu mno katika karine hii.

0 comments:
Post a Comment