NANCHANG, CHINA
23/07/2009.
RAIS wa Umoja wa Vijana wa Jimbo la Jiangxi, Chao Qun Lie, nchini hapa amewataka vijana wa Kitanzania kutumia fursa ya waliyopewa kutembelea eneo hilo kujifunza maendeleo yaliyopatikana katika masuala ya kiuchumi ili waweze kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania.
Akizungumza wakati wa halfa ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Jimbo la Jiangxi kwa vijana wa Kitanzania iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Gloria Plaza, mara baada ya kuwasili Nanchang kwa zaira ya siku tatu ili kuweza ya kujifunza maendeleo mbalimbali.
“Mkiwa vijana wa kizazi kipya mnayo nafasi ya kuimarisha uhusiano wetu kupitia jimbo hili ambalo lina umuhimu mkubwa katika masuala ya kiuchumi kupitia sekta ya kilimo, yakiwemo mambo mengine mfano, kiutamaduni na utalii,” alisema Rais wa jimbo hilo Lie.
Hata hivyo alisema ushirikiano kati ya China na Afrika umekuwa kwa haraka kwani Waafrika wengi wamekuwa wakifika nchini humo kwa ajili ya kubadilishana mawazo katika masuala mbalimbali.
Naye Kiongozi wa Msafara huo, Leornad Musaroche ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shule za Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi alisema, ujumbe huo umefurahishwa na ziara ya eneo hilo, ambalo ni maarufu kwa mapinduzi ya jimbo na nchi hiyo.
Alisema ujumbe huo kwa kutembelea eneo hilo, kupitia Tengwang Pavilion eneo ambalo linatumika kuwaburudisha watu wa ngazi za juu kuhusu na wageni kuhusu historia ya kale kwa njia ya michoro na burudani za kiasili, umeweza kutambua mchango wa watu maarufu waliotoa michango yao kwenye masuala mablimbali yakiwemo ya uandishi na utamaduni.
0 comments:
Post a Comment