Moja ya majengo yaliyojengwa katuika viwango vya hali ya juu na kampuni ya Jiangxi Geo- engineering Group Corporation(JGGC) nchini China
NA MAGRETH KINABO, MAELEZO NANCHANG , CHINA
KAMPUNI inayoshughulika na ujenzi, utafiti na uchimbaji wa madini ijulikanayo kwa jina la Jiangxi Geo- engineering Group Corporation(JGGC) iliyoko China imeahidi kuendeleza ushirikiano zaidi na Tanzania katika shughuli inazozifanya.
Hayo yalisemwa na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hong Wenzhong wakati akizungumza na ujumbe wa vijana kutoka Tanzania walio kwenye ziara ya siku tatu katika mji wa Nanchang , ili kujionea shughuli mbalimbali za kiuchumi, kilimo, madini,kiutamaduni na utalii
Wenzhong alisema tangu kuanzishwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na China kumekuwa na mafanikiano ya ujenzi wa barabara na kuahidi kuudumisha.
“Tumeanzisha ushirikiano mzuri na Tanzania , hivyo tumeweza kujenga barabara, pia tutaimarisha ushirikiano zaidi katika siku za baadae,” alisema Mkurugenzi Mkuu Wenzhog.
Akizungumzia kuhusu suala la madini alisema JGGC ni wazalishaji wakubwa wa madini aina ya shaba katika bara la Asia kupitia jimbo la Jiangxi ambalo limejaliwa na utajiri wa aina mbalimbali za madini yakiwemo ya uranium na silver.
Alisema kampuni hiyo ilianzishwa Mei, mwaka 1958 inahusika na miradi ya uchimbaji madini ambapo ipo katika nchi ya Tanzania , Namibia , Msumbiji , Mexico , Bolivia na Iran .
Wenzhong aliongeza kwamba kampuni yake imeajiri wafanyakazi 21,000 na kwa upande wa Tanzania ina wataalamu wahandisi takribani 20 wanaoendelea kutekeleza miradi mbalimbali.
Naye mtaalamu wa miamba na madini (geologist) Howard Hua, akitoa maelezo kuhusu ramani ya mgawanyiko wa madini nchini humo kwa ujumbe huo alisema China aina ya madini 3,600, ambapo 336 yanapatikana katika jimbo la Jiangxi .
“China ni nchi pekee duniani inayozalisha madini ya Scheelite, Naye Mkuu wa msafara wa vijana hao,ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shule wa za Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Leonard Musaroche, aliishukuru kampuni hiyo kwa michango yake ya ujenzi wa barabara na uchimbaji madini,ambayo yanaongeza thamani katika maendeleo ya taifa letu.
Kampuni hiyo pia inashughulika na ujenzi wa nyumba na viwanda, nchini Tanzania, imeshakalimsha ujenzi wa barabara kubwa zenye urefu wa kilomita 108 ya Shelui- Nzega mkoani Tabora na kilomita 120 ya Kyamyorma - Kiairayombo, hivi sasa inaendelea kujenga barabara yenye urefu wa kilomita 105 ya Sumbawanga - Mpanda.

0 comments:
Post a Comment