New Habari (2006) Limited wadhamini washiriki Miss Vodacom Tanzania 2009!!

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Udhamini na Matukio wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Petter Mwendapole akibadilishana mkataba wa udhamini wa shindano la Miss Tanzania na mkurugenzi wa Lino Agency waandaji wa michuano hiyo, Hashimu Lundenga wakati wa hafla iliyofanyika jana makao makuu wa New Habari, Sinza Dar es Salaam.

KAMPUNI ya New Habari (2006) Limited, imejitokeza kudhamini shindano la Vodacom Miss Tanzania mwaka 2009.Akizungumza leo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya kampuni hiyo, Sinza, Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano, Udhamini na Matukio wa New Habari, Petter Mwendapole alisema udhamini wao utagharimu kiasi cha sh milioni 80. “Hizi ni fedha ambazi zitahusisha mambo mbalimbali ikiwemo matangazo na promosheni ya shindano lenyewe, hapa tunazungumzia pia mavazi kama Tops, fulana na kofia kwa washiriki na watu mbalimbali,” alisema.

Mwendapole alisema kampuni yao imeamua kudhamini shindano hilo katika kuunga mkono juhudi za kampuni ya Lino International Agency kusaidia kumuwezesha binti wa Tanzania kujitegemea. Miss Tanzania inadhaminiwa kupitia gazeti la Bingwa ambalo hutoka kila sikuMbali ya hilo amesema lengo la kampuni hiyo ni kuhakisha utalii wa ndani unakuwa na kupitia magazeti yao watasaidia kutangaza vivutio mbalimbali.
Katika kuhakikisha shindano hilo linawafikia watu wengi, Mwendapole amesema watakuwa na kurasa maalum kwa ajili ya Miss Tanzania na pia watakuwa na matoleo maalum ya shindano hilo.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga na Meneja Huduma kwa wateja wa Vodacom, Elihuruma Ngowi waliipongeza New Habari kwa udhamini wao na kueleza kuwa wana uhakika shindano la mwaka huu litakuwa na nguvu zaidi.New Habari ni wachapishaji wa magazeti ya Bingwa, Mtanzania, Dimba, The African, Rai, Weekend African na Mtanzania Jumapili..

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment