MELI YA MIZIGO YALIPUKA NA KUWAKA MOTO BANDARINI!!

Meli ambayo ahikufahamika mara moja kama ni ya mizigo ama ni ya uvuvi imelipuka na kuanza kuwaka moto wakati ikiwa imetia nanga katika bandari ya Dar es alaam leo asubuhi huku juhudi za kuzima moto huo zilizokuwa zikifanywa na boti ndogo za kuzima moto kutoka kikosi cha zimamoto cha Bandari zikiwa ngumu kutokana na uwezo mdogo wa Boti hizo kusukuma maji ya kuzima moto kuelekea eneo la tukio, kadiri boti hizo zilivyokuwa zikijaribu kuzima moto katika meli hiyo na moto ulikuwa ukizidi kuwaka kitu kilichoonyesha uwezo mdogo wa kikosi hicha kuhimili matukio ya moto kwa vyombo vya baharini.
Mmoja wa wafanyakazi wa Bandari ambaye alikuwepo katika eneo la tukio na ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema kuwa inasemekana meli hiyo ilinunuliwa na mfanyabiashara Bakhressa na ilikuwa ikifanyiwa matengenezo madogomadogo, ndipo ikatokea hitilafu katika mfumo wa umeme kitu kilichosababisha ilipuke moto, hata hivyo bado jeshi la polisi na Mamlaka ya Bandari hawajatoa taarifa yoyote mpaka sasa taarifa zaidi tutawaletea baadae.
Wakazi wa maeneo mbalimbali wakiangalia jinsi meli hiyo ilivyokuwa ikiungua kwenye bandari ya Dar es alaam asubuhi hii.

Moto uliendelea taratibu huku moshi akitanda eneo zima la posta ya zamani.

Hapa ikiendelea kuungua baada ya kulipuka moto

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment