WALIOFANYA VIZURI KATIKA MAUZO SERENGETI BREWERIES WALAMBA TIKETI ZA NDEGE!!

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti Mzee Mark Bomani katikati, akiongea na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya New Africa leo, wakati kampuni hiyo ilipokabidhi tiketi za ndege za kwenda Dubai na Malasia kwa wateja wake waliofanya vizuri kote nchini kwenye mauzo ya vinywaji vinavyozalishwa na kampuni hiyo, Jumla ya Dola za Kimarekani 60.000 zimetumika katika kuandaa safari hiyo kwa washindi hao na watakaa huko kwa siku tano wale wanaokwenda Dubai na wale wanaokwenda Malasia watakaa kwa siku sita, Serengeti inazalisha vinywaji aina ya Serengeti Lager, Stella Artois, Kiki na Vita Malt kinywaji kisichokuwa na kilevi, katika picha kulia ni Shantanu Chitgopkar Mkurugenzi wa masoko na mauzo na kushoto ni Meneja Uhusiano Teddy Mapunda.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Serengeti Breweries Ltd Teddy Mapunda akiongea na wanaghabari ili kufafanua zaidi juu ya zawadi ya tiketi za ndege ambazo kampuni hiyo imeamua kuwazawadia wateja wake baada ya kufanya vizuri katika mauzo ya vinywaji vya kampuni hiyo tiketi hizo ni za kwenda Dubai na Malasia.

Mrs Restituta Godlisten Ndosa kutoka Morogoro akipokea tiketi yake ya ndege kwenda Dubai kwa siku tano na kurudi Dar kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Serengeti Brewers Ltd Mark Bomani leo kwenye Hoteli ya New Africa Restituta ni miongoni mwa wateja wa kampuni hiyo waliozawadiwa baada ya kufanya vizuri katika kuuza vinywaji vya kampuni hiyo.

Wateja wa wakuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti kutoka shemu mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa kamuni hiyo baada ya kukabidhiwa tiketi zao za ndege kwenda Dubai kwa siku tano na kurudi Dar na kwenda Malasia na kwa siku sita na kurudi Dar, wateja hao wwamepewa zawadi hiyo ya Tiketi kutokana na utendaji wao bora kwa kampuni hiyo hafala hiyo imefanyika katika Hoteli ya New Africa leo.





You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment