Mshindi wa kwanza wa mashindano ya kumsaka mrembo wa Miss Dar Indian Ocean atazawadiwa sh. 700,000, jiko la umeme lenye thamani ya ash. Laki sita na shopping yenye thamani ya sh. Laki tano kwa ajili ya mashindano ya kanda ya Kinondoni.
Mashindano hayo yamepangwa kufanyika Ijumaa, Juni 12 kwenye ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip na yatashirikisha warembo 11. Warembo hawa walikuwa kambini chini Miss Morogoro mwaka jana, Suzy Fernandus.
Muandaaji wa mashindano hayo, Jackline Mafuru wa Jackies Collections alisema jana kuwa mshindi wa pili atapata sh, 400,000 na decoder kutoka DSTV ambapo mshindi wa tatu atapata sh. 300,000.
Mshindi wa nne na watano watapata sh. 200,000 na sh. 150,000 ambapo warembo wengine watapata kifuta jasho cha sh. 100,000 kila mmoja.
Mgeni rasmi wa mashindano hayo atakuwa mbuge wa Kinondoni, Mheshimiwa Idd Azzan na bendi ya Machozi chini ya Lady Jaydee itapamba shindano hilo.
Burudani nyingine ni Barnaba na Pipi na kwa mara ya kwanza, wasanii kutoka Nigeria, Ufuneka na Umutola watafanya shoo katika mashindano hayo. Pia kutakuwa na burudani ya ngoma za asili na mazingaombwe.
Kitongoji hicho kimetoa warembo kadhaa ambao wamewahi kutwaa taji la Miss Tanzania miaka ya hivi karibuni, huku Nancy Sumari ambaye alishinda taji hilo mwaka 2005, aliweza kutwaa taji la Mrembo wa Dunia Kanda ya Afrika (Miss World Africa 2005).
Lengo kubwa la mwaka huu ni kurudisha hadhi ya kitongoji cha Dar Indian Ocean baada ya kupoteza taji hilo mwaka jana. .Mashindano ya Miss Dar Indian Ocean yamedhaminiwa na Vodacom Tanzania, Redd’s, City Garden, Golden Tulip, SS Makuwe, Pinacolada Saloon, Jambo Publisher, Regency Hotel, Raque Photo shoot, Asia Idorous Fashion, Multichoice Tanzania na Clouds FM.

0 comments:
Post a Comment