Na Anna Nkinda – Maelezo
11/6/2009 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete jana (juzi) aliwaongoza mamia ya wakazi wa jijini Dar es Salaam katika mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uchumi na Kilimo (SUKITA) Mzee John Kolos Kapinga aliyefariki ghafla jumamosi iliyopita nyumbani kwake Kimara.
Wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Mzee Rashid Mfaume Kawawa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi.
Akitoa mahubiri wakati wa ibada ya misa ya marehemu Prior Father Erasto Mgani alisema kuwa ni jukumu la kila mtu aliyepo hai kujiombea yeye mwenyewe kabla mauti hayamkuta.
“Ni muhimu hivi sasa wakati uko hai kujenga tabia ya kuwa na amani na Mungu kwa kukumbuka kufanya sala kila siku ili siku ya kufa kwako itakapofika uwe tayari”, alisema Father Mgani.
Akisoma historia ya Marehemu ndugu wa familia hiyo alisema kuwa Mzee Kapinga alifariki ghafla asubuhi ya tarehe 6/06/2009 baada ya kudondoka bafuni kwani mkewe alimuacha akiwa mzima kabla hajakwenda katika shughuli za Jumuia ndogondogo ya Parokia ya Mavurunza lakini baada ya kurudi ndipo alimkuta mume wake akiwa amedondoka bafuni.
Aliendelea kusema kuwa marehemu alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Mbinga na hatimaye shule ya Sekondari ya Liwule Mukono Uganda na masomo ya juu ya shule ya sekondari katika shule ya Valentine huko Mombasa Kenya,Marehemu Kapinga katika uhai wake alipata mafunzo ya shughuli za biashara na uongozi wa mashirika na makampuni katika vyuo mbalimbali vya nje na ndani ya nchi. Alipata mafunzo ya siasa katika chuo cha kivukoni.
Elimu na mafunzo hayo yalimwezesha kufanya na kumudu vyema kazi za uongozi katika taasisi alizokabidhiwa kama Agip Tanzania Limited, COSATA, UAC, STC, DABCO na SUKITA katika miaka mbalimbali ya uhai wake.
Marehemu Kapinga ambaye alizaliwa mwaka 1941 katika kijiji cha Ngima wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ameacha mke, watoto wanane na wajukuu watano alizikwa nyumbani kwake Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mwisho

0 comments:
Post a Comment