Kundi la TMK Wanaume Halisi linatarajia kukwea pipa kuelekea Mashariki ya kati nchini Dubai kwa maonyesho kadhaa imefahamika, akiongea na Tovuti ya FULLSHANGWE kiongozi wa kundi hilo Juma Kassim maarufu kama (Sir Nature) amesema wamepata mwaliko kutoka kampuni ya Consult LB Tard Ltd ya nchini humo.
Sir Nature amesema wanatarajia kuondoka tarehe 3 mwezi Julai kwa ajili ya kufanya maonyesho hayo, ambapo wanatarajia kufanya onyesho la kwanza kwenye ukumbi wa DEIRA nchini humo.
Juma Nature ameongeza kuwa wao kama TMK Halisi wamepata faraja sana kupata mwaliko huo kwani unadhihirisha uwezo wao kimuziki na kwamba wanakwenda Dubai kufanya mambo makubwa na mashabiki wao wa huko watasimulia mara baada ya maonyesho yao kwani TMK Halisi imejipanga kukata kiu ya mashabiki vilivyo ikiwa ughaibuni.
Wasanii wa kundi hilo wanaoondoka ni watano nao ni Kiongozi wa kundi hilo Sir Juma Nature mwenyewe, Rich One, Dollo, Stopper na msanii mpya wa kundi hilo anayekwenda kwa jina la KQ Son,Sir Nature ameongeza kwamba maonyesho mengine zaidi yanatarajiwa kuongezeka zaidi mara baada ya kufanya onyesho lao la kwanza nchini humo FULLSHANGWE inawatakia kila la Kheri katika safari yao hiyo ya Ughaibuni, hebu kafanyeni kama mwenzenu Ally Kiba ambaye alikwenda nje kwa onyesho moja na sasa ameng'ang'aniwa huko Ulaya kama Kashikwa na Luba Ziwani vile au sio wadau.






0 comments:
Post a Comment