MJOMBA MPOTO KUPAA ZAKE UFARANSA AKIWAKILISHA NCHI KATIKA SHINDANO LA WASHAIRI DUNIANI!!

Mwimbaji na Msanii wa nyimbo kwa kutumia Mashairi Mrisho Mpoto maarufu kama (Mjomba)akighani wimbo wake wa Mjomba, wakati alipoongea na waandishi wa habari leo jijini juu ya safari yake ya kwenda Nchini Ufaransa, kwa ajili ya kushiriki shindano kubwa la wanamashairi Duniani kote linalojulikana kama The Third Slam Poetry World Cup, litakalofanyika nchini humo kuanzia tarehe 16 mpaka 21 Juni 2009.
Mrisho Mpoto ataimba Shairi hilo kwa kiswahili na kutafsiriwa kwa lugha za kiingereza na Kifaransa , zaidi ya nchi 16 zitashiriki katika shindano hilo ambazo ni Austria, Canada, Denmark Finland, France, Germany, Holland, Madagascar, Quebec, Spain, Swaziland Sweden, Tanzania, Uingereza, Marekani na Zimbabwe, Safari ya Mrisho Mpoto inadhaminiwa na Ubalozi wa Ufaransa na Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa jijini Dar kinachoitwa ALLIANCE FRANCAISE.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment