Kampuni ya King Promoters inayoandaa shindano la kumtafuta Mrembo wa kitongoji cha Chang’ombe jijini Dar es Salaam Vodacom Miss Cahng'ombe 2009 imeshatangaza siku ya shindano hilo, shindano hilo linatarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii Juni 12, 2009 katika ukumbi wa TCC Chang’ombe Dar es Salaam kuanzia saa 2 usiku ambapo warembo 12 wataopanda jukwaani na wote wapo katika hali ya kiushindani kila mmoja akitamba kuibuka na taji hilo kwa mwaka huu.
Kundi zima la FM Academia wazee wa Ngwasuma chini ya uongozi wake Nyoshi El Saadat Sauti ya samba litatumbuiza katika shindano hilo ambapo warembo kumi na wawili watapanda jukwaani kuchuana vikali kutokana na warembo wote kujiandaa vema.
Warembo hao tangu mei 25 mwaka huu walikuwa katika mazoezi makali chini ya Mwalimu wao Vumilia Wilbroad, Matron wao Teddy Chilala na Mwalimu wa shoo kabambe Yahaya Miraji.
Zawadi zitakazotolewa kwa washingi ni kama ifuatavyo; Mshindi wa kwanza yaani Miss Chang’ombe Voda com 2009 atajinyakulia sofa makini kabisa yenye thamani ya shilingi laki tano, Mshindi wa pili atajipatia fedha taslim shilingi laki tatu, Mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi laki mbili, wa nne shilingi laki moja, wa tano shilingi elfu 80 na wengine waliobaki watazawadiwa kiasi cha shilingi elfu arobaini kila mmoja.
Nachukua furs hii kuwashukuru wadhamini wakuu wa shindano hili ambao ni Kampuni ya simu ya Vodacom ambao wamefanya juhudi kubwa katika shindano hili, pia nawashukuru Kampuni ya Bia Tanzania TBL kupitia kinywaji chao cha REDD’S, wengine ni Kampuni ya Art in Tanzania, Tesco Fenicha, Screen Masters, Zizuu Fasion, Gazeti Football, Ikizu Motel, CXC AFRICA N. na Teddy Saloon. Asanteni, warembo waytakaoshiriki katika shindano hilo ni
Ajumy Mussa. (19), Mwengi Ally (19), Frediana Moris (19), Saida Juma (18),
Lilian Bilungi (22), Eva Julius (22), Jamila Othman (22), Salome Mshana (19)
Fatma Yasin (22), Winfrida Fredrick (19), Subira Suleiman.

0 comments:
Post a Comment