BALOZI MWAPACHU MGENI RASMI MISS NORTHERN ZONE!!


Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Juma Volter Mwapachu amethibitisha kuwa Mgeni Rasmi katika usiku wa Shindano la kuwatafuta walimbwende wa Kanda ya Kaskazini Juni 26.
Shindano hilo la Urembo ngazi ya Kanda litafanyika siku ya Ijumaa katika Ukumbi wa Naura Springs Hotel, uliopo eneo la sanawari mataa jijini Arusha kuanzia saa mbili usiku. Limeandaliwa na CROWN INTERNATIONAL ENTERTAINMENT.
Warembo kumi na mbili (12) ambao ni washindi wa Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga watapanda jukwaani kuwania Umalkia wa Kanda ya kaskazini sanjari na tiketi ya kuiwakilisha kanda hii katika mashindano ya taifa (Vodacom Miss Tanzania 2009)
Msanii anayetikisa anga la burudani kwa sasa na single yake inayoshika “missing my baby” maarufu kwa jina la pii pii, Lawrancew Malima aka Marlaw, Binti uzao wa THT Mwasiti na Mabingwa wa Dancing kundi la Contejaz toka Arusha ndio watakaotoa burudani katika kulitia nakshi shindano hilo.
Hadi sasa wadhamini waliothibitisha kutia mkono wa Udhamini ni Vodacom, Tanzania Breweries kupitia kinywaji baridi cha Redd’s Original, TanzaniteOne Ltd, Naura Springs Hotel, Clouds Fm, Ivory Staff Inn Kimandolu, Sacha Motel Namanga na Golden Touch Salon-Kaloleni.
Wengine ni pamoja na duka maarufu la nguo pande za Arusha JJ Black, CET garden, New Habari Ltd kupitia magazeti yake ya Michezo ya Bingwa na Dimba, Via via Restaurant (Meeting Place), Milan Cable Networks na Blogu ya FULL SHANGWE.
Bado milango ipo wazi kwa makampuni/taasisi/ na wadau wengine wote wa fani ya urembo kutuzamini ili kuliboresha zaidi shindano hili.
Warembo wote wataingia kambini siku ya Ijumaa tarehe 19 Juni. Hii ikiwa ni kutoa nafasi kwa Waandaaji wa Mikoa ya Kilimanjaro na Manyara kufanya mashindano ya mikoa yao weekend hii.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment