DAWASCO YAWATAHADHARISHA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM!!.

wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa kazini.
Na Aron Msigwa- MAELEZO.
9/6/2009 Dar es salaam.
Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es salaam (DAWASCO) limewatahadharisha wakazi wa jiji wanaotumia huduma za maji kuwa makini na watu mwanya waowarubuni wananchi kwa kujiita wafanyakazi wa shirika hilo (vishoka) na kuwaunganishia maji kinyume cha sheria.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Afisa uhusiano wa DAWASCO Bibi Marry Lymo kufuatia malamiko ya ya baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu.
Amesema kwa sasa shirika hilo linaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuwaepusha na matatizo mbalimbali yanayoweza kuwapata likiwemo suala la kukatiwa maji na pia kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kutokana na kuunganishiwa maji kinyume cha sheria.
Ameongeza kuwa kwa sasa wafanyakazi wa shirika hilo wanaozunguka mitaani kuwahudumia wananchi wanavitambulisho na pia vizibao vyenye nembo ya DAWASCO
Amefafanua kuwa kwa sasa kuna miradi ya maji inayofanywa na DAWASCO kwa kushirikiana na makampuni mengine ya wawekezaji ili kusogeza huduma ya maji karibu na wananchi na mradi umeshaanza kwa maeneo ya Kimara na Mbezi Beach.
Kuhusu gharama za uunganishaji maji katika maeneo hayo ya miradi ambako kazi ya uunganishaji mabomba inaendelea Bibi Marry amewaomba wananchi kuwa makini ili waepuke ulipaji wa gharama zisizo za lazima kutokana na baadhi ya watu wanaojiita mafundi wa Shirika hilo (vishoka)kutumia mwanya huo kuendelea kuhujumu miundombinu ya shirika hilo kwa kuwaunganishia maji kiholela.
Pia amezitaja changamoto mbalimbali zinazolikabiri shirika hilo likiwemo la wananchi kutolipa bili kwa wakati na hivyo kukwamisha maendeleo ya shirika hilo akiyataja maeneo ya Mbezi beach, Masaki, Oyerstabay, Boko , Magomeni, Sinza na Kibamba kwa kuwa na madeni mengi ya maji.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment