MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES ALAAM PROF. HAROUB OTHMAN AMEFARIKI DUNIA!!

Marehemu Prof. Haroub Othman kulia akiwa na Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda katika moja ya shughuli zake za kitaifa.
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es alaam Prof. Haroub Othman amefariki dunia leo asubuhi huko Unguja akiwa usingizini

Mtoto wa marehemu Tahir Othman amethibitisha kutokea kwa msiba huo mkubwa kwa wasomi wote nchini na Watanzania kwa ujumla, amesema alikutwa amekufa lakini jana alilala akiwa na afya njema kabisa, habari zaidi zinasema marehemu Prof. Haroub alihudhuria uzinduzi wa tamasha la nchi za jahazi usiku wa kuamkia leo, Mungu ailaze pema roho ya Marehemu Amin

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment