BENKI YA STAMBIC YAMWAGA MISAADA YA MAGODORO NA VITANDA WAMA!!

Mwenyekiti wa WAMA mama Salma Kikwete akiongea na wageni waliohudhuria hafla ya Stanbic Bank kukabidhi msaAlign Leftada wa magodoro 100 na vitanda 50 uliotolewa kwa shule ya sekondari Magindu iliyoko Chalinze,Pwani.
Mke wa rais mama Salma Kikwete akikabidhi magodoro yaliyotolewa na Stanbic Bank kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Magindu iliyoko Chalinze, Pwani.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati Taasisi yake ya WAMA ilipokabidhiwa Magodoro 1oo na Vitanda 50 na Benki ya Stambic, vifaa vyote vina na thamani ya shilingi milioni nane na vimetolewa kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Magindu iliyoko Kibaha Mkoani Pwani, wengine katikapicha ni Mkurugenzi wa Benki ya Stambic Bashir Awale kati na mwisho ni afisa masoko wa benki hiyo Abadallah Singano wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye Ofisi za WAMA jijini.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea msaada wa magodoro 100 na vitanda 50 kutoka kwa mkurugenzi wa Benki ya Stambic Bashir Awale, makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za Tasisi ya WAMA inayosimamiwa na mama Salma Kikwete mwenyewe.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment