SERENGETI YAMWAGA KOMPYUTA NA SIMU KWA WATEJA WAKE WALIOFANYA VYEMA KWENYE MAUZO!!

Bwa Sirvestre Ngubi wa Mkongwe Store duka la vinyaji lililoko Vingunguti akibeba zawadi yake ya kompyuta kubwa ya mezani, mara baada ya kuipokea kutoka kwa mwenyekiti wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Marck Bomani leo asubuhi kwenye Hoteli ya New Africa,
Marck Bomani alikabidhi zawadi mbalimbali kwa wateja wa kampuni hiyo waliofanya vizuri katika mauzo ya vinywaji vinavyozalishwa na kampuni hiyo, vinyaji hivyo na kampuni hiyo ni Serengeti Lager, The Kiki, Stella Artois na Vita Malt Plus, Meneja uhusiano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda amewaambia waandishi wa habari kwamba zawadi hizo kwa ujumla zina thamani ya shilingi mliloni 170.
Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Marck Bomani akimkabidhi zawadi ya kompyuta ya mkononi (Laptop computer) Bi. Jane Mawole wa Mawole Store iliyoko Mbezi Beach ambaye ni mmoja wa wateja wa Kampuni hiyo waliofanya vizuri katika mauzo ya vinywaji vinavyozalishwa na kampuni hiyo hafla ya kukabidhi zawadi hizo imefanyika kwenye Hoteli ya New Africa leo asubuhi.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment