Hii ndiyo nembo ya michuano hiyo mwaka huu wa 2009
Timu ya Taifa ya Gambia chini ya umri wa miaka 17 wakishangilia baada ya kuibuka mabingwa mwaka 2005
Timu ya Taifa ya Gambia chini ya umri wa miaka 17 (The Baby Scorpion) wamefanikiwa kuwa mabingwa wapya wa Afrika katika mchezo wa fainali uliofanyika jana nchini Algeria baada ya kuwavurumisha wenyeji Algeria kwa magoli 3-1.
Gambia ilifanikiwa kuongoza katika kipindi cha kwanza baada ya kupata magoli mawili huku Algeria ikijitutumua kwa kurudisha goli moja lilifungwa kwa njia ya penati.
Kipindi cha pili Gambia iliongeza goli la tatu hivyo kuifanya timu hiyo kuwa na uhakika wa kuibuka na ushindi baada ya kuwa mbele kwa magoli 3-1 , magoli mawili ya Gambia yalifungwa na mshambuliaji Ebrima Bojang na goli la tatu lilifungwa na mchezaji wa timu hiyo Alasana Camara.
Hii ni mara ya pili kwa timu hiyo kuchukua ubingwa wa Afrika chini ya umri wa miaka 17 ambapo mwaka 2005 walishinda kombe hilo na kujihakikishia kushiriki katika fainali za Under 17 world cup na kuifunga Brazili katika moja ya michezo yake iliyocheza.
0 comments:
Post a Comment