Msanii wa siku nyingi na mkomavu katika muziki wa Bongofleva Jafari Mshamu aka (Jaffarie) yuko mbioni kudondosha Albam yake mpya itakayokwenda kwa jina la Wali Nazi ambayo itakuwa na nyimbo kumi na mpaka sasa amesharekodi nyimbo tano ambazo ni unapenda nini, Jaffarie, Msijisahau, Saa nyingine na Yeye mimi.
Jaffarie amesema kwa sasa tayari ameshadodondosha pini ya kwanza iliyomo katika albam hiyo ambayo inaitwa unapenda nini katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini na imeshaanza kubamba vilivyo, ameongeza kwamba hivi karibuni anatumaini kuwa kila kitu kitakuwa kimekamilika katika kazi nzima ya kurekodi na atakuwa tayari kuingiza Albam hiyo Sokoni.
Ameongeza kuwa karibu nyimbo zote nne zimerekodiwa katika studio za Lamaa Records zilizoko jijini isipokuwa nyimbo moja ambayo amerekodi kwa producer Said Commorien wa hapa jijini pia ambayo inaitwa Yeye Mimi, ameongeza kuwa pia kwa sasa anaendelea na utengenezaji wa video yake mpya ya unapenda nini ambayo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni tayari kwa kuisanbaza kwenye vituo vya Televisheni
Jaffarie anasema video hiyo imetengenezwa na Studio za Kallage Picture, producer akiwa John Kallage katika video hiyo ambayo picha zake nyingi zimepigwa kwenye Hoteli ya Golden Tulip katika ufukwe wa Bahari ya Hindi pia amemshirikishwa msanii Fatma ambaye ni dada yake na msanii mwingine wa Bongfleva maarufu na anayejulikan kama Hardmad.
Pia katika nyimbo zingine amewashirikisha msanii Malow na Mwanamuziki maarufu kutoka Nairobi nchini Kenya kutoka kundi la Nesesary Noise ambaye pia ni dada yake na Jaffarie mwanamuziki huyu ni mkomavu katika muziki kwani ameshawahi kuimba nyimbo kadhaa na wanamuziki wakali Afrika mashariki kama vile Bebe Cool kutoka uganda ambaye aliimba naye nyimbo inayoitwa Fire ikabamba kisawasawa mtu wangu
Hebu wadau tusikilizie ni mambo gani makubwa ambayo Jafarrie anataka kutuletea mwaka huu katika gemu hii tafu ya muziki wa Bongofleva FULLSHANGWE inamtakia kila mafanikio katika kukamilisha Albam yake hiyo ya Wali nazi.
0 comments:
Post a Comment