Kapt. Deo Mwanambilimbi akimtambulisha rasmi kwa mashabiki wa bendi yao mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Mamaa Hilda Malugara kwenye ukumbi wa Rainbow jana wakati wa onyesho la Valentine ambalo pia lilikuwa ni maalum kusherehekea Bendi hiyo kutimiza miaka miwili toka ianzishwe ambapo mkurugenzi huyo aliwashukuru mashabiki na wadau wote ambao wamefanikisha bendi hiyo kuendelea kwa mafanikio makubwa, alitoa pia shukurani kwa wanamuziki wote wa bendi hiyo kwa moyo wao wa kujituma katika kazi na uvumilivu kwani kila kitu hakiwezi kukosa matatizo, hivyo akawataka kuendelea na moyo huo ili wasonge mbele na kupata mafanikio zaidi.
Bendi ya kalunde imefanikiwa kutoa Albam yake ya kwanza inayojulikana kama Uchona ambayo ilifanya vizuri sana katika ulimwengu wa muziki lakini pia bendi hiyo sasa inaandaa Albam nyingine itakayokwenda kwa jina la nataka nizae na wewe.FULLSHANGWE inawatakia mafanikio makubwa katika kazi yenu ya kuburudisha kuelimisha na kuonya ili jamii yatu iendelee kuwa jamii yenye kuheshimiana na kupendana, kwa picha zaidi za matukio ya jana katika viwanja vyote ambavyo FULLSHANGWE ilivinjari na Camera yake shuka chini upate uhondo zaidi.
Hawa ndiyo Vimwana wa Kalunde Band wakiwa wamepozi mbele ya Camera ya FULLSHANGWE wakati wa onyesho lao lililofanyika kwenye ukumbi wa Rainbow Mbezi Beach katika kusherehekea siku ya wapendanao, lakini pia bendi hiyo ilitimiza miaka miwili toka ianzishwe kuanzia kulia ni mamaa Debora Nyange Meneja wa bendi, Kalunde, Hawa Kasomo,Queen Vero na Rola Maganga.
Kapt. Deo Mwanambilimbi na Queen Vero wakicheza kwa pamoja katika onyesho ambalio liliwa sisimua wengi kutokana na wanenguaji walivyokuwa wakionyesha mambo makubwa katika unenguaji wao Queen Vero na Kalunde wamerejea hivi karibuni tu kutoka Falme za kiarabu ambako walikuwa wakifanya kazi za kimuziki.
Mwanamuziki mualikwa wa bedi ya Kalunde Kasaloo Kyanga akiimba huku akiwa amekaa chini akimwangalia mwanamuziki mwenzie Hawa Kasomo anayecheza mbele yake bendi hiyo ilifanya onyesho katika ukumbi huo jana katika kusherehekea siku ya wapendanao Valentie Day
0 comments:
Post a Comment