VODACOM FOUNDATION DAY YAADHIMISHWA KWA KUMWAGA MISAADA MAHOSPITALINI!!

Mganga mkuu Hospitali ya Temeke Dk. Asha O. Mahita akipokea msaada wa kitanda kwa ajili ya kujifungulia akina mama wajawazito na mashuka kutoka kwa Gaudensi Ansi mkuu wa kitengo cha mauzo kampuni ya Vodacom leo, Vodacom imetembelea Hospitali mbalimbali za wilaya jijini na kutoa misaada katika kuadhimisha siku ya Vodacom Foudation, wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Chriss Blackburn mkuu wa kanda ya Mashariki Vodacom,Imelda Thomas Muuguzi mkuu magonjwa ya nje Hospitali ya Temeke na Mwamvua Mlangwa meneja uhusiano Vodacom kwa picha zaidi shuka chini mdau upate uhondo.
Mohamed Karambo wa Vodacom hakuwa nyuma naye alishirikiana na wenzake katika kutoa zawadi kwa wagonjwa mbalimbali ambao ni akina mama wajawazito.
Dada Stella Ndosi akiwa amembeba mtoto mchanga aliyezaliwa katika hospitali ya Temeke huku akimuangalia wanaomwangalia mtoto katika picha kutoka kulia ni mfanyakazi wa Vodacom Agness Msaki,Sister Mashauri wa hospitali hiyo na Mwamvua Mlangwa meneja uhusiano Vodacom.

Jamani kulea kuzuri! kama unavyomuona dada Agness Msaki wa Idara ya fedha katika kampuni ya Vodacom akimlaza mtoto mchanga ambaye amezaliwa katika hospitali ya Temeke wakati kampuni ya Vodacom ilipotembelea hospitalini hapo na kutoa msaada wa kitanda cha kujifungulia akina mama wajawazito na mashuka katika kuadhimisha siku yao ya Vodacom Foundationa.




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment